
Nembo rasmi ya mamlaka ya Chakula na dawa TFDA.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibati kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.
"TFDA isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan viwanda vya kuzalisha dawa ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda. TFDA mnawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi mara wanapokuwa wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali mapema", amesema Ummy.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA ), Agnes's kijo amesema wanawajibu wa kuimarisha afya za watanzania na kuimarisha maabara zao kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.