
Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Aidha, Mh. Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent kwa ajili ya kikao na baadae majira ya saa tisa au kumi taarifa rasmi ya serikali itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.