Serikali ya mkoa wa Mwanza imetangaza vita dhidi ya wahalifu wanaojihusisha na mauaji ya walemavu wa ngozi na kusababisha hofu kubwa kwa watu wenye ALBINISM ambao wameshindwa kufanya kazi za maendeleo wakihofia usalama wa maisha yao baada ya kuibuka kundi la wahalifu la kupora watoto wadogo wenye ulemavu wa ngozi na kuwanyofoa viungo vya miili yao kutokana na imani potofu za kishirikina.
Tamko hilo limetolewa na kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza Mchungaji Baraka Konisaga katika hospitali ya rufaa Bugando baada ya kumuona majeruhi aliyevamiwa na wahalifu nyumbani kwake katika kijiji cha Ilelema kata ya Ipalamasa wilayani Chato mkoani Geita BI.ESTER JONAS ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza.
Kwa upande wake mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Bugando PROF KIEN MTETA amesema uongozi wa hispitali hautamtoza gharama za matibabu BI.ESTER JONAS na kwamba kumeanzishwa kampeni maaluma ya kuhamasisha jamii itambue umuhimu wa kuwalinda walemavu wa ngozi ambapo Agineta Mtatebwa amesema hali ya mgonjwa inaendelea vizuri anaweza kukaa, kula chakula laini na kuzungumza.