Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (Stamico),Zena Kangoyi
Akizingumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wa STAMICO Bi. Zena Kangoyi amesema wapo katika hatua za mwisho za zabuni ya kumpata mwekezaji mbia kwa ajili ya kutekeleza miradi minne mmoja ukiwa ni kuzalisha makaa ya mawe toka tani laki 1 na Nusu Mpaka laki tatu kwa mwaka,
Miradi mingine ni pamoja na kujenga mtambo wa kufua umeme wa megawati 200 pamoja na kujenga njia ya kuusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti400,
Aidha Bi. Zena amesema shirika hilo limeongeza mapato yake toka million 281 mpaka bilion 3.17 mwaka wa fedha 2014/15 .