Wednesday , 28th Sep , 2016

Serikali imetakiwa kuhakikisha kuwa na itikadi thabiti katika kutekeleza sera zilizowekwa na waasisi wa taifa katika kuondoa ujinga, maradhi na umasikini ili kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wake.

Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (Kulia)

Hayo yamezungumzwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, katika Mhadhara wa tatu wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao ulikuwa unazungumzia elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika.

Jaji Warioba amesema kuwa sasa Tanzania imekosa sera madhubiti ya kiitikadi na kutegemea zaidi matukio na watu na kusema endapo kutakuwa na sera itikadi madhubuti itasaidia kulipeka taifa mbele katika maendeleo.

Amesema vijana wengi wanaimba wimbo wa kutaka maendeleo kwa kuimba wimbo wa kufuta ujinga, maradhi na umasikini bila kujua waasisi wa taifa walitumia mbinu gani katika kufanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi.