Tuesday , 27th Sep , 2016

Nchi za Kusini mwa Afrika zimegawanyika kuhusu pembe za faru na meno ya tembo wakati Mkutano wa Kimataifa wa 17 wa Biashara ya Wanyama walio hatarini kutoweka na mimea ukianza wiki hii, Sandton, Jijini Johannesburg.

Tembo wakiwa katika hifadhi

Nchi za Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia zinaomba ridhaa ya chombo cha Kimataifa kuziruhusu kuuza hazina kubwa ya meno ya tembo waliyoyakamata, wakati Namibia ikitaka hatua ya kuzuia uuzaji wa meno hayo ya tembo iendelee.

Pia kumekuwa na mgawanyiko juu ya suala la uuzaji wa pembe za faru, ambapo Waziri wa Mazingira wa Zimbabwe, Oppah Muchuinguri akisema nchi yake inaungwa mkono na mataifa mengine ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).