Nchi wanachama wa jumuiya ya kusini mwa Afrika (SADC), zinatarajia kushiriki maonesho ya wakulima ya nanenane kwa mwaka ujao wa 2017, ili kubadilishana uzoefu miongoni mwao hatua ambayo inatajwa kuwa itawaletea tija wakulima wa nchi hizo sambamba kupanua wigo wa kujitangaza kupitia mazao wanayozalisha.
Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Maoneshi ya wakulima katika mikoa ya Nyanda za juu kusini AMOSS MAKALLA, amesema hayo wakati akifunga kikao cha pili na cha mwisho cha maandalizi ya maonesho ya wakulima yanayotarajiwa kuzinduliwa Agost Mosi, katika viwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.
MAKALA ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Mbeya ametumia fursa hiyo kuiagiza Sekretarieti ya Maandalizi ya Maonesho ya sikukuu ya wakulima, katika mikoa ya Nyanda za juu kusini, kuandaa mazingira kwa ajili ya kuwapokea washiriki kutoka nchi za SADC.
