Tuesday , 12th Jun , 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amejitolea kadi 220 za Bima ya Afya zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 11 kwa watoto yatima na waishio Kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu mwaka mzima ikiwa ni sehemu sadaka kwa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mh. Makonda amesema kwamba kupitia kadi hizo zitawawezesha watoto hao kupatiwa matibabu bure kwa kipindi cha mwaka mmoja katika hospitali yoyote hapa nchini. 

"Kwa kawaida Mwezi wa Ramadhani watu wamekuwa wakifuturisha watoto yatima lakini inakuwa ni chakula cha siku moja kwaiyo katika mwendelezo wa mwezi mtukufu ni vyema niguse maisha ya watoto yatima kwa kuwapatia uhakika wa matibabu  kwa kuwapatia Bima ya Afya. Kwa sasa tumeanza na watoto 220 na baadaye tutaongeza wengine" Makonda.

Aidha wakati akitoa kadi hizo, Mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba watoto hao  waliopatiwa kadi hizo hawahusiani na wale waliojitokeza kwenye zoezi la kutafuta haki ya mtoto.