Rais wa Chama cha Mawakili nchini, Charles Rwechungura .
Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Chama cha Mawakili nchini, Charles Rwechungura kwenye uzinduzi wa wiki ya msaada wa kisheria iliyozinduliwa katika viwanja vya mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.
Rwechungura amesema iwapo mamlaka husika zinazoshughulika na masuala ya ardhi zitatimiza majukumu yake ipasavyo madai yaliyoko katika mahakama mbalimbali nchini yatapungua kwa kuwa mashauri mengi yaliyoko mahakamani yanahusiana na ardhi.
Kwa upande wake mwakilishi wa mwenyekiti wa chama cha mawakili nchini Grace Dapa, amewataka mawakili kuwafikia wananchi walioko vijijini ambao wanahitaji msaada mkubwa wa kisheria kwa kuwa mawakili wengi wako mijini na kuwasahau watu wa vijijini ambao hawajui kama kuna watu wa kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada wa kisheria.