
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Samwel John Sitta Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 11,2016
Mhe. Sitta alifariki dunia tarehe 07 Novemba, 2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani.
Mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umeagwa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam ambapo Viongozi wengine waliojumuika kuuaga mwili huo ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri wakuu wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi Mhe. Ferdinand Katipwa Wambali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Rais Mstaafu wa awamu awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiaga mwili wa Marehemu Samwel John Sitta Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 11,2016
Baada ya kuagwa katika viwanja vya Karimjee, mwili wa Marehemu Samuel John Sitta umesafirishwa kwenda Dodoma ambako Wabunge, Viongozi wa Mkoa na wananchi walipata fursa ya kuuaga katika Viwanja vya Bunge na baadaye jioni utasafirishwa kwenda Tabora ambako maziko yatafanyika kesho Jumamosi huko Urambo.
Rais Mstaafu wa awamu awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Wiliam Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa wakiaga mwili wa Marehemu Samwel John Sitta Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 11,2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt . John Pombe Magufuli akimfariji Mama Margareth Sitta, Mjane wa aliyekuwa Spika Mstaafu Marehemu Samwel John Sitta alipoongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa kiongozi huyo mkongwe katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Oktoba 11, 2016