Sunday , 28th Jan , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo ametia saini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa mwili Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es Salaam

Mhe. Rais Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pia wametoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Mama Maria Kisanga na kufanya maombi ya pamoja na familia ya marehemu

Jaji Mstaafu Robert Kisanga alifariki dunia tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.