Monday , 28th Apr , 2014

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete akikabidhi vitabu kwa jeshi la wananchi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Kikwete amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha.

Maktaba hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.

Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.