Akiwa katika ofisi hizo Rais Magufuli aliyekuwana Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasilina Utalii Meja Jenerali Gaudensi Milanzi ameshuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa kati ya jana IjumaanaleoJumamosiJijini Dar es Salaam.
Aidha, Dkt. Magufuli ameoneshwa magari yaliyokamatwa yakiwa yamebeba pembe hizo na watuhumiwa wanane wanaodaiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya pembe za ndovu.
Rais Magufuli amewapongeza askari wote waliopo katika Kikosi Kazi cha kudhibiti na kupambanana biashara haramu ya pembe za ndovu pamoja na Raia wema wote wanaotoa ushirikiano katika operesheni hiyo na amewahakikishia kuwa anatambua kazi kubwa wanayoifanya na anawaunga mkono.
“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya na ninawahakikishia kuwa ninawaunga mkono, chapeni kazi, wakamateni wote wanaojihusisha nabiashara hii haramu, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa au nani, kamateni, walamsijali cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake, sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka watu wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe ili tuokoe wanyama wetu ambao wanaendelea kutekelezwa.
“Hapa mmekamata pembe 50 maana yake tembo 25 wameuwawa, haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwasababu ya watu wachache wenye tama ya kutaka utajiri wa haraka haraka”amesisitiza RaisMagufuli.





