
Msikiti huo wa al-Rawda ulioko katika mji wa Bir al-Abed ulipigwa bomu na kusababisha waumini kutawanyika na kuanza kushambuliwa kwa risasi.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo ambalo linaelezwa kuwa baya tangu wanamgambo wa Kiislaam walipoongeza mashambulizi yao katika rasi ya Sinai mwaka 2013.
Mwezi Septemba, takriban polisi 18 waliuawawa baada ya wanamgambo hao kushambulia msafara wao karibu na mji wa al – Arish