Sunday , 31st Jul , 2016

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) amezitaka Radio za jamii kuhamasisha usafi wa mazingira nchini.

Naibu Waziri Mpina ametoa kauli hiyo alipokuwa akishiriki siku ya usafi kitaifa, mwishoni mwa wiki wilayani Masasi Mkoani Mtwara.

Akiongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara katika majumuisho ya ziara yake Wilayani Masasi, Naibu Waziri Mpina aliwataka viongozi wa mkoa huo kuunda sheria ndogondogo za mazingira zitakazo watoza faini wananchi waharibifu wa mazingira mkoani humo, na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na hali ya wananchi ili waweze kujifunza na kujijengea tabia ya usafi.

Aidha Mpina amewataka wananchi walio na tabia ya uchomaji moto misitu kuacha kwa kuwa uchomaji moto taka nao siyo njia nzuri ya uondoshwaji wa taka, hivyo kuwe na miondombinu rafiki kwa uondoshwaji wa taka, na kiongozi wa mkoa ambaye hatakuwa tayari kushughulikia usafi wa mazingira na yeye awe tayari kushughulikiwa