Friday , 1st Jul , 2016

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwigage amesema Serikali imedhamiria kuvifufua Viwanda vya nguo vilivyokufa nakuanzisha vingine vipya kwa lengo la kuzuia na kupiga marufuku uingizwajwi wa nguo za mitumba nchini.

Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwigage amesema Serikali imedhamiria kuvifufua Viwanda vya nguo vilivyokufa nakuanzisha vingine vipya kwa lengo lakuzuia na kupiga marufuku uingizwajwi wa nguo za mitumba nchini.

Waziri Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na East Africa Radio nakuongeza athma kubwa ya Serikali ni kuhakikisha viwanda vya nguo nchini vinazalisha kwa ubora na kiwango kikubwa ili kulingana na ushindani wa soko la dunia.

Amesema Serikali imeamua kupiga marufuku ya uingizwajwi wa nguo za mitumba nchini kuanzia mwaka 2019 kwasababu hadi kufikia mwaka huo tayari viwanda vitakua vinazalisha nguo zenye ubora.

Hata hivyo waziri Mwijage amesema mpaka sasa Tanzania inaviwanda 8 tu ambavyo vinazalisha bidhaa hiyo ya nguo kwa kusuasua kwasababau ya changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la ukosefu wa umeme wa uhakika na viwanda hivyo vimekua vikizalisha chini ya kiwango.

Ameongeza katika kushughulikia swala hilo lakufufua viwanda litaenda sambamba nakutengeneza ajira kwa watanzania wengi kwaajili ya kuzalisha kwakua viwanda vilivyopo kwa sasa vinazalisha kwa asilimia 30 mpaka 40 ikiwa ni chini ya malengo ya taifa.

Amewataka wakulima wapamba nchini kuacha udanganyifu wakuharibu Pamba kwa kwa makusudi kwa lengo lakuongeza uzito wa bidhaa hiyo.