Tuesday , 26th May , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetangaza rasmi ratiba ya uchaguz ikiwa ni pamoja na tarehe ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mataafu Damian Lubuva amesema uteuzi wa wagombea urais, wabunge na madiwani utafanyika Agosti 21.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kampeni rasmi za uchaguzi zitafanyika kwa miezi miwili kuanzia Agosti 22 mwaka huu na zitaishia Oktoba 24 ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi.

Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimekuwa vikilalamikia tume hiyo kuchelewesha kwa makusudi kutoa ratiba ya uchaguzi huku vikidai tume hiyo ililenga kukibeba chama tawala kujipanga kwanza.