Tuesday , 23rd Jul , 2019

Kutokana na mwingiliano mkubwa wa kibiashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, upo uwezekano mkubwa wa ugonjwa wa Ebola kusambaa  zaidi kutoka na mwingiliano wa watu.

Ugonjwa wa Ebola

EAC kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano kwa Umma, Richard Owora imezitahadharisha nchi za EAC, kupeana taarifa ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari ambao umeibuka katika Jimbo la Ituri nchini Congo, lililopo umbali wa kliomita 70 mpakani mwa Congo DR na na Sudani Kusini.

''Matukio ya mlipuko wa Ebola katika nchi za EAC yaligundulika kwa mara ya kwanza kwa wagonjwa watatu nchini Uganda, Juni mwaka huu na Serikali ya Uganda ilijitahidi kuudhibiti kwa wakati'', imesema taarifa ya Owora.

Aidha ikumbukwe kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa tangazo kwa Umma kuhusu hali ya tahadhari inayopaswa kuchukuliwa hatua za dharula na kwamba jamii ya Jumuiya ya nchi hizo inapaswa kushirikishwa ipasavyo hususani wananchi waishio mipakani.