Monday , 31st Mar , 2014

Jeshi la Polisi mkoani Pwani, nchini Tanzania limesema limefanikiwa kupata maiti ya mtu mmoja katika ajali ya kuzama kwa mtumbwi jana usiku huko Rufiji mkoa wa Pwani.

Habari za kupatikana kwa mwili huo zimethibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich Matei ambaye amesema mwili huo ni wa mtoto mdogo na kufafanua kuwa ajali hiyo ni ya Mtumbwi kugongana na Pantoni inayotoa huduma katika mto huo.

Kamanda Matei amefafanua kuwa katika ajali hiyo watu wanane walizama katika mto Rufiji na kwamba jitihada za kuwatafuta watu wengine saba wanaohofiwa kufa maji zinaendelea.