
Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba ambapo amesema serikali itajenga magereza katika maeneo yenye shughuli za Kilimo ili Shughuli ya kurekebisha tabia iendane na Uzalishaji.
Mhe. Mwigulu amesema kuwa mkakati huo ni pamoja na kuwahamisha Wafungwa ambao wameshahukumiwa katika magereza ya mijini na kuwahamishia maeneo yatakapojengwa magereza kwa ajili ya kwenda kutumikia vifungo huku wakiendelea na shughuli nyingine za Ujenzi wa taifa.
Katika hatua nyingine amewataka maafisa Masuhuri kuelekeza fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kulipia huduma mbalimbali ikiwemo Umeme katika taasisi za kiserikali ili kuepuka changamoto zitakazoweza kujitokeza pindi huduma hizo zitakapositishwa kutokana na kutokulipa kwa wakati.