MwenyekitiI wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM), mkoani Mbeya Amani Kajuna
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kajuna amesema kati ya asilimia 60 ya vijana wa jiji la Mbeya ni asilimia 19 pekee ndio wenye uhakika wa vibarua ambapo waliosalia hawana kazi kabisa.
Amesema kuwa tatizo la ajira kwa vijana limekuwa sugu nchini ukiwemo mkoa wa Mbeya hivyo anahitajika mtu anayeliona suala hilo kwa mapana na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.
Aidha amesema atawajengeo uwezo watoto yatima kuhakikisha kuwa wanapata mahitaji yote ya msingi ya binadamu ikiwemo haki ya kupata elimu.
Hata hivyo Kajuna ameongeza kuwa akipata ridhaa kutoka kwa wananchi atawapigania wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama (wamachinga), kuhakikisha wanapatiwa maeneo ambayo yanafaa kwa biashara zao ili waweze kujikimu kimaisha.