Wednesday , 14th Oct , 2015

Chama cha walimu nchini (CWT ),Kimesema kuwa kama Mwalimu Julius Nyerere Kambarage angekuwepo maisha ya walimu yasingekuwa magumu kama yalivyo katika kipindi hiki.

Rais wa chama cha walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

Hayo yamesemwa leo na Rais wa Chama hiko Gration Mukoba wakati akiongea na East Africa Radio na kuongeza kuwa wao kama waalimu wanamkumbuka sana baba wa Taifa ambaye aliishi maisha ya kiualimu na hakuwa mbinafsi na kwamba aliwajali sana walimu.

Mukoba ameongeza kuwa hata pengo la mshahara kati ya walimu na watendaji wengi wa serikali lilikuwa dogo wastani wa 1 kwa 5 tofauti na sasa ambapo ni wastan wa 1 kwa 30.

Aidha Mukoba amesema walimu wanakabiliana na changamoto nyingi za kimazingira na kazi na kuhoji kwanini wabunge wanaofanya kazi miaka mitano wanalipwa mamilioni ya fedha huku walimu wakilipwa mafao kidogo na hata malipo yake hucheleshwa sana.