Sehemu ya nyumba iliyobomoka
Wakizungumza na EATV katika eneo la tukio lililopo barabara ya 18 jijijni Tanga viongozi wa serikali na wale wa wananchi wa eneo hilo wamesema limetokea majira ya saa 11 Alfajiri wakati mvua iliyoambatana na upepo ikinyesha ndipo ukuta wa nyumba hiyo uliojengwa na mawe makubwa ya baharini ulipodondoka na kusababisha madhara hayo.
Waliokufa katika eneo hilo wametajwa kuwa ni Bakari Shabani mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Ngamiani kati na Hassan Abdala mwenye umri wa mwaka mmoja ambao walifariki papo hapo huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya akiwemo mama mzazi wa marehemu ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo.
Kufuatia hatua hiyo diwani Mbaruk ameiomba halmashauri ya jijij la Tanga pamoja na idara ya majengo kufanya ukaguzi wa majengo chakavu hasa katika kipindi hiki cha mvua za masika ili baadhi ya familia ziweze kuhamishwa na kutafutiwa mahali pa kujisitiri ili kuepuka maafa makubwa dhidi ya wahusika.