Waziri wa Maendeleo ya mifugo Dr. Titus Kamani.
Watafiti na wataalam wa nje na ndani wakiwemo wa kutoka Chuo Kikuu Cha Kimataifa cha Sayansi Cha Nelson Mandela wamesema jitihada za ziada za kuepusha mwingiliano wa wananchi, mifugo na wanyamapori zinahitajika na tafiti zinaonesha kuwa magonjwa yanayoshambulia binadamu ambayo chanzo chake ni wanyamapori yanaongezeka mfano ugonjwa wa ebola.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi Dr. Titus Kamani amekiri kuwepo kwa tishio hilo na kwamba licha ya changamoto zilizopo serikali inaendelea kuchukua tahadhari za kuzikabili likiwemo la migogoro inayopelekea mwingiliano wa wanadamu na wanyamapori .
Baadhi ya wananchi wakiwemo wafugaji wamesema hawaoni jitihada za dhati za kutatua migogoro iliyopo badala yake kinachofanyika ni kuibuka makundi ya watu wanaoendelea kutumia migogoro kupora rasilimali zilizopo na kuwaacha wafugaji wakiendelea kukabiliwa na masikini.