Mashine ya kuchuja damu kwa wagonjwa wa figo.
Hayo yamebanishwa Jijini Dar-es-Salaam na Mkurugenzi wa Huduma za uuguzi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Agnes Mtawa wakati alipokuwa akipokea msaada wa mashine ya kusafisha damu kutoka ubalozi wa India, mashine ambayo inathamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi za Tanzania.
Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto ya uchache wa mashine za kuchuja damu, pia kuna uhaba mkubwa wa madaktari bingwa wa magonjwa ya figo ambapo kwa sasa wapo madaktari saba tu huku wengine watatu wakiwa wapo nje ya nchi kwa ajili ya kupata elimu zaidi.