
Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua na Sikio wa Hospitali Muhimbili Dk. Edwine Loyombo wakati wa utoaji mafunzo ya utunzaji wa vifaa hivyo kwa wazazi na watoto wanaotumia vifaa hivyo lengo likiwa ni kuhakikisha vifaa hivyo vinaleta matokeo chanya kwa watoto hao na kupunguza tatizo hilo nchini.
Amesema tatizo la watoto kuzaliwa na usikivu hafifu ni kubwa kwa sasa nchini na linasababishwa na matumizi ya baadhi ya dawa za chanjo kipindi cha ujauzito kwa mama na kuwataka kinamama kuwa makini na chanjo na matumizi ya dawa pindi wanapokuwa wajawazito ili kuzuia tatizo hilo.
Kwa mujibu wa Dkt. Loyombo amesema seti ya kifaa cha kusikia kimoja kinauzwa Shilingi Milioni 27 na oparesheni yake hufanywa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 3 kulingana na hospitali husika.
Tazama video hapa chini ikieleza habari kamili.