Kukamwatwa kwa Ahmed ambaye anasoma shule yaMacArthur High School, kumeibua hisia nyingi huku wengi wakisema ni uonevu kutokana na mtoto huyo kuwa na asili ya Kiarabu na kwa kuwa ni Muislam, hivyo kuamua kuanzisha kampeni ya kumtetea iliyopewa jina la "I Stand with Ahmed" ambayo ilikuwa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
Rais Obama wa Marekani nae aliamua kuunga mkono kampeni hiyo kwa kuandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa saa hiyo ni nzuri na kumuuliza iwapo anataka kuipeleka Ikulu, na kuhimiza watoto wengine kupenda sayansi kwani ndicho kinachoifanya nchi ya Marekani kuwa bora.
kwa upade wake Mtoto Ahmed alisema alitengeneza saa hiyo ili akamuonyeshe mwalimu wake, lakini alihuzunishwa baada ya mwalimu huyo kudhani ni bomu hivyo kuripoti polisi.
Baba wa mtoto wa huyo Mohamed Elhassan Mohamed ambae asili yake ni nchini Sudan, alimsifia mtoto wake huyo na kusema ana kipaji kikubwa sana kwani ndiye anayetengeneza kila kitu nyumbani kwao ikiwemo komputer na simu yake ikipata hitilafu.
Mtoto huyo aliachiwa baada ya saa hiyo kufanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa haikuwa na kihatarishi chochote kiusalama.



