Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya, Noeli Chocha,
Rais huyo wa Afrika kusini alikamtwa mwaka 2010 mwezi Novemba, akiwa na gari ndogo wakati ikvuka mpaka wa Tanzania na Zambia, mjini Tunduma akidaiwa kuelekea Jijini Dar es Salaam akitokea Afrika kusini ambapo alikuwa na Mke wake Anastazia Elizabeth.
Mwanamke huyo ambae nae alishikiliwa na jeshi la Polisi alikuwa mjamzito wakati huo ambapo alijifungua mtoto wa kike wakati akiwa Mahabusu ambae kwa sasa ana umri wa miaka mitano ambapo mwanamke huyo ameachiwa huru na mwanae baada ya kubainika kuwa hana hatia.
Akisoma Hukumu Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Mbeya, Noeli Chocha, amesema Vuyo Jack,asmekutwa na hatia baada ya kukutwa na dawa za kulevya aina mbalimbali kilo 34.66 kwenye gari yake.
Jaji Chocha ametoa hukumu hiyo baada ya kuiendesha kuwa muda wa miaka 6 ambapo pamoja na mambo mengine pia gari yake aina ya Nissan Hard Body iliuzwa na Mahakama na fedha kuingia serikali.
Kwa upande wake wakili aliekuwa akimtetea mtuhumiwa huyo, Wakili wa Kujitegemea Ladslaus Lwekanza amesema ameridhika na hukumu ya mteja wake huyo na kusema kuwa hiyo ni adhabu tosha kwa mujibu wa sheria endapo mtu akibainika bila shaka yoyote endapo atakutwa na madawa ya kulevya.