Wednesday , 4th Feb , 2015

Kamati ya Uongozi ya Bunge na Serikali imekaa kikao cha Dharula kujadili suala la uandikishaji wa wapiga Kura kwenye daftari la kudumu la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa kieletroniki BVR, zoezi ambalo limeshaanza katika baadhi ya mikoa nchini.

Mh. James Mbatia

Kamati ya Uongozi ya Bunge na Serikali imekaa kikao cha Dharula kujadili suala la uandikishaji wa wapiga Kura kwenye daftari la kudumu la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa kieletroniki BVR, zoezi ambalo limeshaanza katika baadhi ya mikoa nchini Tanzania.

Akitoa hoja ya Kujadiliwa suala hilo kama jambo la dharula kwa taifa Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia amesema zoezi hilo limeanza bila kuwashirikisha wadau ambao ni vyama vya siasa jambo linaloashiria kukiuka utaratibu na makubaliano yaliyofikiwa.

Mbatia amesema Tume ya Uchaguzi ilikubaliana na vyama vya siasa kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania kwamba Tume hiyo itakuwa ikiwashirikisha kwa kila hatua, lakini cha kushangaza, tume hiyo imeanza zoezi hilo bila kuwashirikisha ikizingatiwa kwamba tume hiyo ilishasema kuwa haina pesa za kutosha.

Mbatia amesema “….Jambo hili ni muhimu lijadiliwe ili kuliepusha taifa letu na machafuko wakati wa uchaguzi kama ilivyotokea kwa mataifa mengine.... ikizingatiwa kuwa muda uliobaki kabla bunge hili halijavunjwa tuingie kwenye uchaguzi ujao ni miezi kama mitano au sita hivi”

Akijibu hoja hiyo ambayo iliyotaka bunge liahirishe Shughuli zake Mwenyekiti wa Bunge Mh. Mussa Azzan ameitisha kikao cha dharura kwa kuitaka Serikali kupitia wizara ya Fedha, kamati ya Uongozi ya Bunge na mtoa hoja (Mbatia) kukutana kuanzia muda huu ili kulipatia suluhu suala hilo.

Kwa mujibu wa Mbatia, mikoa ambayo tayari Tume ya Uchaguzi imeanza taratibu za uandikishaji ni Mtwara, Ruvuma, Lindi na Njombe.