Thursday , 14th Jul , 2016

Mkoa wa Tabora umeripotiwa kuwa na changamoto mbalimbali wa kutozingatia uzazi wa mpango na mimba za utotoni zinazosababishwa na mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu changamoto za huduma ya afya zinazoukabili mkoa wa Tabora

Akizungumzia suala hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba amesema hatua hiyo imeendela kukwamisha juhudi mbalimbali za serikali mkoani humo katika kuboresha sekta za Afya hususani maeneo ya vijijini.

Dkt. Kamba amesema kuwa changamoto kubwa ya mkoa huo ni mimba za utotoni ambazo kwa kiasi kikubwa ndio wanasababisha uwepo wa vifo vingi vya watoto wa chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora kuacha kuzaa watoto wengi ambao wanashindwa kuwahudumiwa.

Nae Afisa Muuguzi Msaidizi katika zahanati ya Ivia Mjini Tabora, Zipora Enock amesema uzazi wa mpango bado ni changamot kubwa katika maeneo mengi ya Mkoa wa Tabora.

Sauti ya Mganga mkuu mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba