Mkurugenzi wa Utafiti Kanda ya Kaskazini Bw.January Mafuru
watafiti wa kilimo wanasema wamebaini kuwa virusi hivyo vinavyosababisha magonjwa ukiwemo ugonjwa wa batobato kali na michirizi kahawia vinasambazwa na nzi mweupe ambapo mazao yanayoshambuliwa na ugonjwa huo yanakosa uwezo wa kuzaa lakini pia mihogo inayotoka inakuwa haifai kwa matumizi ya chakula.
Ni kutokana na tishio hilo watafiti wa zao la muhogo kutoka nchi ishirini na tatu ulimwenguni wanakutana jijini Arusha kwenye kongamano kujadili njia sahihi za haraka za kuchukua kukabiliana na nzi hao weupe
Hata hivyo tayari yapo matumaini kwa wakulima baada ya kituo cha utafiti wa kilimo cha Mikocheni kugundua aina ya mbegu inayokinzana na magonjwa hayo ambayo imeanza kusambazwa kwa wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Pwani.





