Mwanasheria mkuu wa Burundi Valentin Bagorikunda
Mwanasheria mkuu wa Burundi Valentin Bagorikunda amethibitisha kuwa kati ya watu 87 waliouawa katika mashambulizi hayo yaliyotokea mnamo tarehe 11 mwezi Desemba mwaka jana, serikali iliizika miili 58 ya wanaoshukiwa kuwa waasi.
Mwanasheria huyo mkuu wa Burundi amesema watu hao walizikwa katika kile alichokitaja makaburi ya serikali yaliyoko kusini mwa mji mkuu Bujumbura na katika eneo la Mpanda katika jimbo la Bubanza lililiko magharibi mwa Burundi.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameishutumu serikali ya Burundi kwa kujaribu kufunika ukweli kuhusu idadi ya waliofariki katika mashambulizi hayo.