Monday , 8th Feb , 2016

Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, ambaye pia ni afisa intelijensia wa hifadhi hiyo, amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa kuhusika na tukio la utunguaji wa helkopta.

Mhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro, Iddi Mashaka, ambaye pia ni afisa intelijensia wa hifadhi hiyo, amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa kuhusika na tukio la utunguaji wa helkopta namba 88HF na kusababisha kifo cha rubani wake, Rogers Gower, raia wa Uingereza.

Imeelezwa mashaka amekuwa kinara mkubwa wa ujangili katika hifadhi mbalimbali zilizopo kanda ya ziwa kwa kutoa ushirikiano kwa majangili wenzake pamoja na kuwaazimisha silaha za kufanyia ujangili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, kamanda wa polisi mkoani Simiyu, Lazaro Mambosasa, amesema mtuhumiwa huyo ni mwajiriwa wa hifadhi hiyo ya Ngorongoro.

Kamanda Mambosasa amesema jitihada zilizofanywa na jeshi la polisi mkoani Simiyu, zikiongozwa na mkuu wa upelelezi, Jonathan Shana, zimeendesha msako maalum uliowashirikisha askari wa vyeo mbalimbali, kikosi kazi na askari wanyamapori pamoja na wananchi, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wenzake nane walioshiriki katika tukio hilo.