Tuesday , 28th Jun , 2016

Hosptali ya Taifa Muhimbili kitengo cha watoto kimepokea msaada wa vifaa tiba 145 vyenye dhamani ya shilingi za kitanzania milioni 23 kwaajili ya kurahisisha upatikanaji wa matibabu.

Akiongea na waandishi wa habari hosptalini hapo wakati akipokea msaada huo kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita, mkuu wa idara ya watoto Hosptali ya Taifa Muhimbili Dkt. Mary Charles amesema vifaa hivyo vitapunguza foleni ya vipimo kwa watoto na kurahisisha matibabu kwa watoto 300 wanaotibiwa kila siku katika kitengo hicho.

Dkt. Mary amesema vifaa vilivyotolewa ni pamoja na kifaa cha kupimia joto, kupima mapigo ya moyo na presha pamoja na kupimia uzito na kwamba mahitaji ya vifaa hivyo ni makubwa na kwa sasa watajitosheleza.

Naye daktari mkuu wa Geita Gold Mine Dkt Kiva Mvungi amesema, ni wajibu wa kila kampuni, taasisi na jamii kwa ujumla kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini hivyo msaada huo ni moja ya majukumu ya mgodi huo kwa jamii.

Dkt. Kiva Mvungi ameongeza kuwa mgodi wa Geita Gold Mine umejikita kutoa huduma mbalimbali za afya nchini ikiwemo ya kufanya ukarabati mkubwa wa hosptali teule ya Geita kwa kutumia shilingi bilioni moja za kitanzania, kampeni ya Kili Challenge kwa kushirikiana na TACAIDS na wadau mbalimbali dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa UKIMWI.

Aidha Dkt. Mvungi ameongeza kuwa mgodi huo pia imejenga vituo kadhaa vya matibabu mjini Geita, Nyakabale na Buhongo sambamba na hosptali iliyopo kwenye.