Monday , 30th Jun , 2014

Imeelezwa kuwa mchango mkubwa wa kisera katika uchumi unaofanywa na sekta binafsi unastahili kuku

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi nchini Tanzania (TPSF) Dkt Godfrey Simbeye.

Imeelezwa kuwa mchango mkubwa wa kisera katika uchumi unaofanywa na sekta binafsi unastahili kukuzwa kwa manufaa ya sekta na taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya sekta binafsi (TPSF) Dkt Godfrey Simbeye, amesema hayo na kufafanua kuwa aushauri wao kisera unaiweka nchi katika mazingira mazuri ya kibiashara.

Akizungumza wakati wa kufunga rasmi pazia la taaisi inayosaidia ushawishi kaika kuboresha mazingira ya biashara nchini, Simbeye alisema, mchango wa sekta binafsi katika kufanya mazingira ya biashara kuwa mazuri unatakiwa kutiliwa maanani katika ngazi zote za maendeleo kwa manufaa ya umma.

Bei ya samaki katika soko kuu la samaki la Feri jijini Dar es Salaam nchini Tanzania imepanda maradufu kufuatia upepo mkali unaovuma baharini kwa sasa na kusababisha wavuvi kushindwa kuapata samaki.

Wakizungumza na Kurasa leo baadhi ya wafanyabiashara wa samaki katika soko hilo wamesema iwapo hali hiyo itaendelea biashara ya samaki katika soko hilo itakuwa ngumu kwa sababu watalazimika kupandisha bei zaidi tofauti na ilivyo sasa.