Tuesday , 31st May , 2016

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema kwamba Mbunge wa Tarime vijijini John Heche (Chedema) amepewa adhabu ndogo ya kutoshiriki vikao 10 vya Bunge linaloendelea kwa kutii kamati ya Bunge.

Akisoma maamuzi ya Bunge kuhusu wabunge wa upinzani kutotii sheria za bunge kwa kushinikiza kujadiliwa kwa hoja kuhusu bunge kurushwa live, Mkuchika amesema Mbunge John Heche alitoa ushirikiano wa kutosha katika kujibu maswali na kutii maelekezo ya kamati hiyo.

Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Bunge hapo jana liliwasimamisha wabunge 7 wa upinzani kwa kosa la kutotiii sheria za bunge wabunge hao ni Tundu Lissu na Ester Bulaya ambao wamesimamishwa mkutano wa 3 na wa 4, Godbless Lema, Zitto Kabwe, Halima Mdee, Paulin Gekul wamesimamishwa vikao vyote vinavyoendelea wataingia bungeni mwezi wa 9 na John Heche ambaye amesimamishwa vikao 10 vinavyoendelea.