 (1280x853).jpg?itok=wT6W1H34×tamp=1478957499)
Mbunge wa Hai Mh. Freeman Mbowe.
Akizungumza kwenye ibada ya mazishi ya Mh. Samuel Sitta aliyefariki tar 7 Novemba 2016, iliyofanyika Urambo mkoani Tabora, Mh. Mbowe amesema kupatikana kwa katiba ndio jambo la msingi ambalo litadhihirisha kuenzi kazi za Mh. Samuel Sitta, kwani amefariki akiwa bado mchakato wa katiba ambayo aliipigania kwa kiasi kikubwa Bungeni, ikiwa bado haijapatikana.
Mh. Mbowe amesema alipokuwa akiongoza Bunge la Katiba, Mh. Sitta aliendesha Bunge hilo kwa haki bila kujali itikadi ya vyama, akipigania nchi kupata katiba mpya kwa manufaa ya watanzania.
"Mh. Sitta alijitahidi sana kutuweka pamoja katika Bunge lile la katiba, lakini kwa mapenzi ya Mungu kazi ile hakuweza kuikamilisha na amemchukua, taifa linatudai katiba, kumuenzi Mzee Sitta ni kwa kukamilisha suala la kitaba na kuwapa wanachi katiba", alisema Freeman Mbowe.
Freeman Mbowe aliendelea kwa kusema kuwa msiba wa Mh. Samuel Sitta uwe fundisho kwa viongozi wengine na watu wote waliobaki, kuwa wamoja na kujenga taifa lenye mshikamano.
"Tunapokuwa misibani tunakuwa wapole, leo hata askari wetu ambao sisi wengine tunapambana nao, ukiwaangalia leo wana hofu, ukiwaangalia leo wana unyenyekevu, msiba huu uwe fundisho, kujenga mapenzi mema kati yetu, kujenga taifa lililo jema, ili tuwe na taifa lenye mshikamano", alisema Freeman Mbowe.