Friday , 10th Mar , 2017

Watu watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali ambazo ni vipande 9 vya meno ya tembo na mikia 2 ya twiga.

Vipande vya meno ya tembo vilivyokamatwa

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, DCP Dhahiri Kidavashari amesema watu hao wamekamatwa mnamo tarehe 09.03.2017 majira ya saa 3:00 usiku katika msako uliofanywa na polisi kwa kushirikiana na maafisa wa TANAPA katika Kijiji na Kata ya Lupatingatinga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni HUSSEIN KHAMIS ISSA MLAWI na ZACHARIA MUSA wote wakazi wa Kijiji cha Matwiga.

Amesema watuhumiwa hao ni majangili na kwamba upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani.