Wednesday , 17th Sep , 2014

Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania ukiwa na lengo la kuidhinisha aina mpya ya hati ya kusafiria za kielekroniki zikiwemo za kibalozi, za maofisa na za kawaida.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera.

Akizungumza jana Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Makame ambapo amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha

Dkt. Makame amesema mkutano huo unatarajia kupokea na kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, mkoa wa Mara Nchini Tanzania umewataka wafanyabiashara kufungua maduka yao lakini kwa masharti ya kuandika barua ya kuomba kupewa muda usiozidi siku tano wawe wameshanunua mashine za kieletroni za kutolea risiti EFD.

Akizungumza na wawakilishi wa wafanyabiashara mkoani humo meneja wa TRA mkoa wa Mara Bw. Joseph Kalinga amesema TRA imekubali kufunguliwa kwa maduka endapo kila mfanyabiashara atakubali kuandika barua ndani ya siku tano kuanzia leo awe amenunua mashine hizo.

Hapo jana ilishuhudiwa zaidi ya maduka elfu moja yaliyopo katikati ya mji wa Musoma mkoani humo yakifungwa kufuatia mgomo ambao uliitishwa na wafanyabiashara wa manispaa ya Musoma kugomea matumizi ya mashine za kieletroniki za kutolea risiti za mauzo EFD.