Kiwango cha mauzo ya bidhaa za Tanzania katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kimeongezeka ambapo hivi sasa Tanzania inahodhi takribani asilimia ishirini na sita ya bidhaa zote zinazouzwa katika soko hilo kutoka kiwango cha asilimia 18 kilichokuwepo mwaka 2005 wakati soko hilo likianzishwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji na masuala ya fedha kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Bernard Damas Haule, amesema hayo katika mahojiano na Hotmix ambayo ilikuwa inataka kufahamu nafasi ya Tanzania katika soko hilo.
Kwa mujibu wa Bw. Haule, mauzo ya Tanzania katika soko hilo yamepanda kutoka wastani wa dola za Marekani milioni tisini na nane mwaka 2005 hadi wastani wa fedha za Tanzania shilingi trilioni mbili, kiwango alichosema kuwa kimeifanya Tanzania kuwa nchi ya pili inayoongoza katika soko hilo baada ya Kenya