Sunday , 9th Mar , 2014

Chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimetaka kutoruhusiwa kwa mapenzi ya jinsia moja nchini kutokana na uwezekano wa nchi kutomudu madhara yatokanayo na matendo hayo.

Chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimetaka kutoruhusiwa kwa mapenzi ya jinsia moja nchini kutokana na uwezekano wa nchi kutomudu madhara yatokanayo na matendo hayo.

Rais wa MAT Dkt. Primus Saidia, ameyasema hayo na kuonya kuwa mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ngono za kinyume na maumbile zinaweza kusambaza magonjwa ya ukimwi, homa ya ini, kisonono na kaswende.

Kwa mujibu wa Dkt Saidia, magonjwa hayo yana gharama kubwa kwa taifa kuweza kuweza kutoa matibabu yake, ikitiliwa maanani huduma duni za afya zinazopatikana nchini, mfano wa karibuni ukiwa ni jinsi umaskini unavyolifanya taifa lishindwe kutoa matibabu hata kwa magonjwa ya kawaida kama malaria na kipindupindu.