Dr Shein ameyasema hayo alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Amaan katika kilele cha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
''Mapinduzi haya ndiyo kielelezo cha utu wa Mwafrika kuheshimika na kuwa huru katika nchi yake ana wananchi wana kila sababu ya kusheherekea kwani matunda yake yamewanufaisha wananchi wote bila ya kubagua'' Amesisitiza Dr. Shein
Hata hivyo Dr Shein amewakumbusha wazanzibar kuendelea kuwa watulivu wakati Serikali kupitia Tume ya Uchaguzi Zanzibar ikijipanga na kutangaza kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

