Tuesday , 19th Jul , 2016

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven Kebwe amezitaka halimashauri zote za mkoa huo kutenga asilimia 10 ya michango ya mapato ya ndani kuzielekeza katika kusaidia vikundi vya ujasiliamali kwa kinamama na vijana.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt.Kebwe Steven Kebwe amezitaka halimashauri zote za mkoa huo kutenga asilimia 10 ya michango ya mapato ya ndani kuzielekeza katika kusaidia vikundi vya ujasiliamali kwa kinamama na vijana.

Dkt.Kebwe ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum na East Africa Television nakuongeza kuwa sambamba na hilo watahakikisha wanaweka mazingira wezeshi ya ajira kwa makundi hayo kwenye sekta ya Kilimo kwakuwa mkoa huo una maeneo ambayo yanafaa kulimwa kwa ukubwa wa hekta Milion 2.2 ambapo ni hekta laki 7 tuu ndizo zinazolimwa mkoani humo.

Amesema kwa sasa ofisi yake inahimiza wawekezaji wa viwanda katika mkoa huo na kutenga maeneo maalumu na kuwavutia wadau mbalimbali wa uwekezaji na tayari kuna muwekezaji kutoka Ulaya amewekeza katika sekta ya kutengeneza nguo na kuajiri wakazi wa Morogoro zaidi ya watu 500.

Ameongeza kuwa tayari wametenga eneo lenye ukubwa wa Hekta zaidi ya 6000 kwaajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kwakushirikiana na mashirika ya maendeleo kwaajili yakuyaendeleza ikiwa ni pamoja na kujengwa bandari kavu,maduka makubwa na kujenga Hospital kubwa ya rufaa ya mkoa huo wa Morogoro na huduma za kijamii na kuongeza ajira kwa watu wa mkoa wa Morogoro.