Friday , 1st May , 2015

Viongozi wa vyama vya CCM, na CHADEMA wilayani Iringa Mjini wakiitaka manispaa ya Iringa kuongeza matangazo kuhamasisha wananchi kujitokeza zaidi kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mtindo wa kieletroniki BVR.

Afisa Habari wa Manispaa ya Iringa Bi. Sima Bingileki.

Baadhi ya vituo vya uandikishaji vilivyoanza kazi hiyo juzi ambapo kata tano za Kitwiru, Ruaha, Igumbilo, Nduli na Mkimbizi zimefungua zoezi hilo litakaloendelea kwa siku saba kila kata na kukutana na viongozi hao wa kisiasa waliokuwa wanapita kukagua maendeleo ya zoezi hilo na kueleza kuwa mwitikio ni mzuri kwa siku ya kwanza

Akizungumzia zoezi hilo afisa uchaguzi Bw Gabrial Msunza amesema manispaa hiyo yenye jumla ya vituo vya uandikishaji 192 katika kata 21 limegawanywa katika awamu nne na litamalizika siku ya tarehe 30 mwezi wa tano.

Kwa upande wake afisa habari wa manispaa hiyo Bi. Sima Bingileki akieleza kuwa manispaa hiyo inaendelea kufanya matangazo ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwa kutumia njia mbalimbali hivyo hakuna haja ya wadau wa zoezi hilo kuwa na wasiwasi.

Zoezi la uandikishaji wapiga kura linaendelea katika halmashauri zote nne za mkoa wa Iringa ambapo viongozi wa serikali pamoja na vyama vya siasa wameendelea kuwasihi wananchi wa mkoa huu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ambapo katika siku hii ya kwanza kasoro nyingi zilizoonekana awali wakati wa zoezi hilo mkoani Njombe zimeonekana kudhibitiwa na tume ya taifa ya uchaguzi