Thursday , 12th May , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla, amesitisha shughuli zote za kibinadamu zinazofanywa na watu wachache walivamia uwanja wa zamani wa ndege wa Mbeya uliopo katika ya jiji la Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.

Makalla ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea taarifa za uwanja huo kuvamiwa na maafisa ardhi wa jiji la Mbeya kwa madai ya kuuza viwanja kwa baadhi ya wananchi kinyume cha taratibu klwa kanuni na sheria zilizoanzisha mamlaka ya viwanja vya ndege.

Mhe. Makalla amesema kuwa taarifa alizonazo kuwa mchakato wa uuzwaji wa eneo hilo umefanyika wakati hata mamlaka ya uwanja huo haujashirikishwa kikamilifu hivyo akaamua kupiga marufuku zoezi hilo la uuzwaji wa maeneo ya uwanja huo.

Wakizungumza kwa uchungu wakazi wa maeneo hayo wamelalamikia watu kuuziwa viwanja hivyo na kufanya shughuli ambazo hata Mkuu wa mkoa wa awali alipiga maarufu hivyo kumtaka Mkuu huyo wa Mkoa mpya kuanza utaratibu mpya juu ya uwanja huo.

Tatizo la upamaji na viwanja Mkoani Njombe limeonekana kuwa kubwa baada ya kubainika kuwa kuna utoaji wa viwanja vyenye hati halafu kupewa hati nyingine jambo linalozua migogoro mkoani humo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla.