
Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe. Lazaro Nyalandu amethibitisha hayo baada ya kufanya mazungumzo na Shirika la SamaritAn Purse la Marekani na kukubaliana kuwasaidia kupata matibabu watoto hao ambao ni Doreen, Saidia na Wilson kutokana na hali zao kutoridhisha.
"Ndege hiyo itaondoka jioni ya leo kutoka mji wa Charlotte Jimbo la North Carolina nchini Marekani na inatarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kesho jioni, endapo upatikanaji wa hati za kusafiria 'Visa' utafanikiwa kwa siku ya kesho basi wasafiri wataondoka Jumapili asubuhi kuelekea Marekani wakiwa wameongozana na wazazi wao". Alisema Nyalandu
Aidha, Nyalandu ameendelea kwa kusema kwamba baada ya kuwasili Charlotte North Carolina, wagonjwa hao pamoja na waliowasindikiza watasafirishwa kwa ndege maalum ya kubeba wagonjwa yaani Air Ambulance hadi mji wa Soux Jimbo la Lowa ambako watapatiwa matibabu.
.