Monday , 21st Nov , 2016

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuanzia leo Ofisi ya Rais TAMISEMI haina budi kusitisha usajili wa vijiji hadi zoezi la kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu litakapokalimika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. JUmanne Maghembe (Kushoto) na Naibu wake Mhandisi Ramo Makani (Katikati) muda mfupi kabla ya mkutano wake na watendaji wa wizara hiyo kuanza

 

Ametoa kauli hiyo leo wakati akifanya mazungumzo na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

“Kuanzia leo ninasimamisha zoezi la usajili wa vijiji unaofanywa na TAMISEMI hadi wizara ya Maliasili na Utalii ikamilikshe zoezi la kuainisha na kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwa na taifa la walalamikaji,” alisema huku akishangiliwa na watendaji hao.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika wizara hiyo, Bw. Zahoro Kimwaga pamoja na Bodi ya Utalii nchini wabadilike na kuanza kufanya kazi kibiashara zaidi.

“Tumieni mabango ya kieletroniki (electronic screens) kurusha picha za wanyama. Mfano pale nje ya uwanja wa Taifa, au uwanja wa ndege hata kwenye njia kuu  za mikoani wekeni mabango ya iana hiyo.” alisisitiza.

Msikilize hapa Waziri Mkuu.....

Waziri Mkuu akipiga marufuku uanzishwaji wa vijiji vipya
Waziri Mkuu akitoa maagizo kuhusu kuutangaza utalii wa Tanzania