Wednesday , 20th Aug , 2014

Mtafiti wa kilimo wa Selian Rose Ubwe amesema kwa sasa kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa mbegu za mahindi ya viini lishe kutokana umuhimu wa matumi ya mbegu hizo kwa jamii kwa sasa.

Bi. Umbwe amesema kuwa ongezeko la mahitaji ya mbegu za mahindi lishe ni kubwa kutokana nauelewa mkubwa wa faidi za matumizi ya mbegu hizo huku huku upatikanaji wake wa sasa ukikubwa na changamoto kubwa.

Kwa upande wake mmoja wa wasambazaji wa mbegu zenye viini lishe Peter Mutisya amesema kwa sasa kazi kubwa ni kwa mamlaka zinazohusika kuhakikisha kuwa wananchi wanauelewa wa kutosha kuhusu matumiza sahihi ya nafaka za viini lishe

Mradi huo wa usambazji wa teknolojia ya mahindi tayari unatekelezwa katika wilaya za Muheza ,Kilosa,Korongwe na Mikumi.

Katika hatua nyingine, serikali imezitaka Taasisi za Fedha kuacha ukiritimba wa rushwa katika utoaji wa mikopo wa wajariamali wadogo wa kati.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu,Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu wakati wa kongamano la wajasiliamali na Taasisi za Fedha ili kujadili mchango wa upatikanaji huduma hizo katika kukuza uchumi wa nchi.

Dtk. Nagu amesema kuwa mchango wa sekta za fedha katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini siyo wa kubeza hivyo kutaka ushiriki wa wadau wote katika uwekezaji kupitia uwezeshaji unaofanywa na serikali pamoja na taasisi na sekta binafsi.