
Mahakimu hao wamefutwa kazi na Tume ya Kuchunguza Majaji na Mahakimu ambayo imekuwa ikiwachunguza wahudumu wa idara ya mahakama waliokuwa kazini kabla ya Agosti 2010, katiba ya sasa ilipoidhinishwa
Tume ya kuchunguza majaji na mahakimu ambayo ilikuwa na jukumu hilo la kuchunguza idara ya mahakama na wahudumu wake tokea mwaka 2010 na kuwabaini mahakimu hao kwa makosa hayo.
Mwenyekiti wa bodi hiyo Sharad Rao amesema baadhi ya mahakimu hao wanane walijihusisha na ufisadi na wengine hawakuwa na uwezo wa kufanya uamuzi mwafaka.
Aidha, inapendekeza idara ya mahakama ishirikiane na vyuo vikuu kuweka mpango wa kutoa mafunzo zaidi kwa maafisa wanaohudumu katika idara ya mahakama.
Bodi hiyo inatarajiwa kumaliza kazi yake kufikia mwisho wa Machi 2016.
Chanzo BBC