Saturday , 20th Feb , 2016

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza wakurugenzi wote wa manispaa nchini pamoja na maafisa wa elimu kuhakikisha kwamba uskauti haukwami bila ya sababu za msingi.

Vijana wa Skauti wakiwa katika moja ya maadhimisho nchini

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt. Hussein Mwinyi katika maaadhimisho ya siku ya skauti ikiwa ni kumbukumbu ya mwanzilishi wa skauti duniani Sir Lord Robert Stephenson Smyth Baden Powell aliyezaliwa terehe 22 Februari mwaka 1857.

Kwa upande wake Rais wa Skauti Tanzania Profesa Joyce Ndalichako amesema ni wajibu sasa kwa vijana kujiunga zaidi na skauti ili kupata mafunzo ya uadilifu yatakayowasaidia kuwa na maadili mema zaidi na kuipenda nchi yao.